HFC WAANGUKIA PUA. WAKUBALI KICHAPO CHA 3-2 TOKA KWA QUARTERS FC

Highridge FC waangukia pua. Wakubali kichapo cha 3-2 toka kwa Quarters FC

Katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa General Tire jijini Arusha, HFC wamekula kipigo kitakatifu toka kwa mahasimu wao na majirani zao Quarters FC.

Walikuwa ni HFC walioanza kuliona lango la wapinzani wao baada ya kuonana vizuri huku wakicheza kandanda nzuri mithili ya EPL, alikuwa ni Ackrim akicheza wing ya kushoto aliyeonekana kuwapa shida kubwa mabeki wa QFC kwa mbio na mchezo wake mzuri akiwazidi akili na maarifa basi aliachia cross ndogo iliyomkuta Abel RKay aka #TheFlash akiwa takribani mita 25 ama 26 mpaka 27 akamchungulia kipa amekaaje na kuachia shuti la juu lililomshinda kipa na mpira kutinga nyavuni.

Dakika chache baadae, HFC wakapata kona na Abel RKay akaichonga kona fupi na kumpasia Muksini aliyeachia shuti kali na kumbabatiza beki wa QFC na mpira kutinga nyavuni.

Mpira uliendelea kuchezwa huku QFC wakilizakama lango la HFC kwa vipindi na hatimaye wakafanikiwa kupata goli la kwanza.

Kipindi cha pili kila timu ilijaribu kufanya mabadiliko ya hapa na pale lakini yakaleta faida kwa wageni QFC walioweza kusawazisha na kupata goli la tatu.

Man of the match katika mchezo huo alikuwa Abel RKay aliyafanikiwa kufunga goli moja na kutoa assist moja.

Hadi mwisho wa mchezo HFC 2-3 QFC.

Njkiripoti kutoka HFC ni mimi Abel Robins Kalamata, Afisa Habari, HFC.

Comments

Popular posts from this blog

Arthur Ostyn kurudi Ubelgiji kesho. Arthur Ostyn returns to Belgium tomorrow

HIGHRIDGE SCHOOL SPORTS BONANZA. GENERAL TIRE GROUND ARUSHA. TOMORROW JULY 14, 2018 FROM 9 AM