HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG 2. MZIZI WA FITINA HAUJANG'OLEWA
HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG FC 2. MZIZI WA FITNA HAUJANG'OLEWA BADO.
Katika mpambano wa soka wa kirafiki uliozikutaisha timu za HFC na SunFlag FC uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Genwral Tire imeshuhudiwa mbabe akikosekana baada ya timu hizo kulazimishana droo ya 2-2.
Mchezo ulianza kwa kasi sana huku Sunflag Fc wakianza kulisukuma gozi mithili ya club za Arsenal na Barcelona, wakionana kwa pasi nzuri na zenye uhakika wakati huo HFC wakiwa hawana wasiwasi wowote wakiwasoma na kujaribu kuziba nafasi iki wapinzani wao hao wasiweze kuoata penetration yoyote.
Mpira ulichezwa kwa muda mrefu sana hasa maeneo ya katikati huku kila upande ukishindwa kupata nafasi ya kupata goli la kutangulia.
Wakiwa wamefanya mashambukizi ya mara kwa mara, Sunflag Fc kwa kupitia mkjuwa wa penati walikosa goli na hali kurudi ile ile yaani 0-0. Lakini HFC wakiwa wamejisahau hasa walinzi wake, Sunflag fc wakarudi tena langoni kwa HFC na kufanya shambulizi kali mithili ya Vietnamese army na kupitia mchezaji wao machachari #Fadhil wakaandika bao la kwanza.
Haikuchukua muda kwa upande wa HFc akiwa ameingia kuongeza mashambulizi #Papaa aka Didier Drogba aka #Didy alileta uhai kwenye safu ya ushambuliaji akaipatia HFC bao la kusawazisha baada ya kumchungulia vizuri kipa wa Sunflag fc aliyekuwa ameliacha lango lake aka kulitelekeza utadhani alikuwa ameacha kipa msaidizi langoni mwake.
Sunflag wakaendelea kuwa mwiba mchungu mbele ya HFC kwani walizidisha mashambulizi huku wakitumia mwanya wa udhaifu wa back line ya wenyeji wao ambao walikuwa wakijisahau mara kwa mara huku wakishindwa hata kucheza offside tricks na kuwapa mwanya wageni wao ambao kwa kupitia #Rafael wakapata goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Hfc kufanya madhambi langoni mwake.
HFC wakaja juu nao wakati huu wakicheza kwa jihad kubwa wakitaka kuondoa lawama na aibu toka kwa mashabiki wao waliojazana uwanjani kushudia mpambano huo. Hasa wengi wakijitokeza wakitaka kushuhudia free kicks za #TheFlash ambaye leo alifulia ile mbaya kiasi kwamba hata alipoombwa afanyiwe sub aligoma akidhani pengine itatokea Free kick ili nae apate goli kwa ajili ya timu yake. Lakini wahenga wa kisasa wananena kuwa sio kila siku ni Jumapili.
Wakicheza kwa ustaarabu, ujuzi na mbinu zao za juu huku kocha akiwaambia mara kwa mara wacheze mpira aliowafundisha mazoezini, HFC walibadilika ghafla na kuanza kulishambulia lango la wapinzani wao mithili ya jamaa wanaomfukuza mwizi kimya kimya, hatimaye wakafanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa striker aliyeingia kipindi cha pili #Nicoalas aliyeutokezea mpira wa assist iliyopigwa na #Papaa aka Didier Drogba na akamhadaa kipa na kuusweka mpira nyavuni mithili ya afande wa magereza aswekavyo mharifu lupango.
Baada ya hapo kukatokea piga nikupige, kosa nikukose na mashambulizi ya hapa na pale kwa timu zote mbili lakini bila mafanikio.
Man of the match kwenye mchezo wa leo alikuwa ni #ZePapaa aka.Drogba aliyefunga goli la kwanza kwa HFC na kutoa assist kwa #Nicolas aliyefunga goli la pili.
Hadi mwisho wachezo HFC 2, SUNFLAG FC 2
NIKIRIPOTI KUTOKA #PrivateOffice, ni mimi #AbelRKay, Afisa Habari, HFC.
Tukutane tena Ijumaa ijayo panapo majaaliwa. Alamsiki.
Ni shida doi!!!!
ReplyDeleteKivumbi kbs mjumbe. Free kicks za #TheFlash were FI kbs but the ball we had kwa field was even more FI kbs laaah
Delete