SUPER FRIDAY MATCH DAY. HFC vs SOWETO FC. GROUND: GENERAL TIRE, ARUSHA. USIKOSE UHONDO
SUPER FRIDAY MATCH DAY. HFC vs SOWETO FC. GROUND: GENERAL TIRE, ARUSHA. USIKOSE UHONDO Tunapenda kuwaalika wapenzi wa soka kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha kuja kushuhudia mpambano mkali na mtamu wa soka kati ya HFC vs SOWETO FC zote za jijini Arusha. HFC wamejipanga sawa sawia wakiwa na ari, nguvu na nia ya ushindi kuhakikisha mashabiki hawapotezi muda wao bali kushuhudia burudani muruuuwa ya kabumbu safi. Wakiwa chini ya kocha Papaa aka Fidel Castro na kepteni J. Bayo aka mzee Jomo watahakikisha kuwa wapinzania wao hao wanarudi makwao vichwa chini miguu juu mithili ya jogoo aliyechinjwa kwa ajili ya krismasi. Kwa upande wa SOWETO FC, sio timu ya kubeza Kwani wanacheza mpira mzuri na wa upinzani ya hali ya juu. Wana nguvu na speed nzuri sana. Hivyo mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu kwa pande sote na ya kukata na shoka. Karibuni woooote mfurahie burudani babukubwa. #AbelRKay #TheFlash