HIGHRIDGE FC 2 BARAA FC 1
HIGHRIDGE FC 2 vs BARAA FC 1 Katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo jioni jijini Arusha kwenye dimba la General Tire imeshuhudiwa Highridge FC wakiwagalagaza Baraa Fc kwa kuwachapa magoli mawili kwa moja. Mchezo huo uliochelewa kuanza kutokana na kucheleweshwa kwa baadhi ya mambo na waandaaji wa mpambano huo, ulikuwa mkali, mzuri na wa kusisimua huku timu zote mbili zikicheza kwa tahadhari na kasi ya hali ya juu na wakati mwingine rafu za hapa na pale zilionekana kuutawala mchezo kutokana na upinzani mkali uliopo kwa timu hizi mbili. Alikuwa ni Mcdennis Johnston aka Mjumbe mshambuliaji mwenye nguvu na mrefu aliyeiwahi krosi nzuri iliyopigwa na Papaa aka kocha na kuiunga hadi nyavuni. Baraa Fc walipambana na kusawazisha goli hilo na kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu. Kipindi cha pili mchezo ulianza tena kwa kasi ileile huku timu zote zikiwa zimefanya mabadiliko na huzu zikiendelea kufanya mabadiliko. Ndipo akaibuka Mola Jumanne, mshambuliajj machachari mwenye m...