Highridge FC vs Baraa FC Ijumaa Hii. Jipange
Kesho Ijumaa kutakuwa na mpambano wa soka wa kirafiki kati ya Highridge Football Club dhidi ya Baraa Fc kutoka Moshono zote za jijini Arusha.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa General tyre maeneo ya Njiro Arusha unatarajiwa kuhudhuriwa na watazamaji wengi kwani timu hizi mbili ni wapinzani wa muda mrefu sana na umepita muda mrefu tangu wakutane mara ya mwisho.
Mchezo huo pia utatumika kumuaga mwanasoka kutoka Ubelgiji Arthur ambaye amekuwa akiitumikia HFC tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 na sasa amemaliza mkataba wake na atarejea Ubelgiji baada ya wiki moja.
Mara nyingi Baraa FC wamekuwa vibonde wa HFC hivyo kuufanya mchezo wa kesho kuwa ni wa kusisimua na wenye upinzani wa hali ya juu sana. nikiongeza na kepteni wa HFC Eric John Bayo, nilimuuliza anauongelea vipi mchezo huu dhidi ya Baraa FC alisema,
'' Dah huu mchezo kwa kweli si wa lelemama, tunatarajia kupata upinzani mkubwa toka kwa wapinzani wetu, lakini nasi tunaujua mpira kwa hiyo tutakabiliana nao kama ambayo tumekuwa tukikabiliana nao siku zote na kwaweza.''
Elikana Kaliwaski, Eric J. Bayo, Paulinho, Deviski, A.rk, na wengine wakishangilia goli kwenye mojawapo ya mechi zilizowahi kupigwa pale General Tire. Photo kutoka HFC Library.
Abel RKay: Afisa Habari, HFC.

Kama kawa kama dawa, watakula goli za kutosha hawa
ReplyDelete