HIGHRIDGE FC WAANZA MAZOEZI RASMI
Katika harakati za kuimarisha kikosi cha HFC, Club ya Highridge FC leo hii wameanza mazoezi rasmi. Mazoezi hayo yalipaswa kuanza jana jumanne lakini kutokana na mvua kukataa katakata mazoezi yasifanyike basi wana HFC wakajikita leo uwanjani na kufanya mazoezi murua kabisa wakiwa chini ya kocha mchezaji Adam aka Papaa.
Club hii ya HFC watakuwa wanakutana kila wiki Jumanne na Jumatano kwa ajili ya mazoezi na Ijumaa kwa ajili ya mechi, na wiki hii wanatarajiwa kuwakaribisha Super Loaf FC. Mechi kati yao na wageni hao imekuwa na sintofahamu kutokana na kuahirishwa mara kwa mara. Lakini imefahamika kiwa wiki hii mechi kati ya timu hizi mbili lazima ipigwe.
Nilipotembelea mazoezini jioni ya leo katika viwanja vya General tire nimeshuhudia idadi kadhaa ya wachezaji waliohudhuria wakiwa wenye furaha ya mazoezi na wakifanya mazoezi kwa umakini sana wakiwa chini ya Papaa kocha wao mchezaji.
Hao Supa Loaf watapigwa tu, maana Hamna jinsi, na ni wazi kuwa mkate mbele ya chai huwa haukatai
ReplyDeleteNa wamekula kichapo cha dog mwizi leo
Delete