SUPER LOAF FC WAINGIA MITINI. WAKWEPA MVUA YA MAGOLI
SUPER LOAF FC WAINGIA MITINI. WAKWEPA MVUA YA MAGOLI.
Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na pafukapo moshi pana moto. Hili wameliona SuperLoaf FC na kwa kufwatilia misemo hiyo wakaamua kutoonekana uwanjani. Baada ya kula kichapo cha goli 4-2 katika dimba la General tire pale walipowatembelea HFC, SuperLoaf FC walionekana kutoridhika na kipigo hicho na kuomba kurudiana Ijumaa ambayo ingefwatia. HFC hawakuwa na hiana bali kuwakubalia na kusema karibuni tena.
Jana HFC walionekana muda wote wa jioni wakifanya mazoezi ya hapa na pale huku kikosi chao kikiwa kimekamilika vilivyo wakiwa wamejipanga kutoa dozi nyingine. Lakini mazoezi hayo yalionekana kutokuwa na mwisho baada ya habari kusambaa kuwa SuperLoaf FC hawaji uwanjani. Na baada ya kuhoji nikapata.habari kuwa kutokuja kwao uwanjani ilikuwa ni kuhofia mvua. Mvua waliyoiogopa sio ambayo ilikuwa ikinyesha jana asubuhi na mchana la hasha bali waliogopa mvua ya magoli kwa kukumbuka kipigo walichokipata ijumaa iliyopita wakaona bora lawama kuliko fedhea. Wakaweka pozi na kubaki manumbani kwao.
Comments
Post a Comment