SUPER LOAF FC WAPUMULIA MASHINE MBELE YA HIGHRIDGE FC. WACHEZEA KICHAPO CHA 4-2
SUPER LOAF FC WAPUMULIA MASHINE MBELE YA HIGHRIDGE FC. WACHEZEA KICHAPO CHA 4-2
Wahenga walisema mtoto akililia wembe mpe, asiyesikia la mkuu huvunjika guu, na waswahili nao wana msemo wao usemao, hayawi hayawi sasa yamwkuwa. Hayo yamejili leo katika dimba la General tire wakati miamba wawili walipokutana kuvaana kifutiboli kwenye mchezo wa kirafiki kati ya wenyeji Highridge FC vs SuperLoaf FC.
Mchezo ulianza kwa utulivu sana huku kila timu ikijaribu kumsoma mwenzake. Huku referee Musa akionesha madhaifu ya mara kwa mara huku akiwa hana uhakika mara kadhaa kama mchezaji yuko offside ama la.
Walikuwa ni SuperLoaf walioanza kuliona lango baada ya mshambuliaji machachari Hamisi kupokea krosi na kuuweka mpira nyavuni. Goli hilo liliwapatia kichaa HFC ambao walianza kulisakama lango la wapinzani wao kama nyuki huku wakicheza mpira safi na mtamu na mashambulizi yao yakianzishwa na mid fielders Amani na Saidi. Na hatimaye mpira ulimkuta Mustafa beki namba 4 aliyeachia shuti la mbali lililomshinda kipa wa SuperLoaf fc na kutinga nyavuni. Hivyo hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu zilikiwa zimetoshana nguvu kwa kufunbana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na HFC wakifanya mabadiliko kwa kumtoa Paul Tarimo aka Pogba na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph, Gerald Gunza akatoka na McDennis akaingia, Adam David akatoma na akaingia Ackrim na Elikana aka Elikanus akatoka na akaingia Peter Sagas. HFC wakafanyiwa madhambi na kiungo Said akapiga free kick nzuri sana iliyomkuta Peter Sagas aka baba Sydney aka mzee mwenzangu ambaye bila ajizi kwa kutumia uzoefu wake katika soka akaugusa tu kidooogo na kuusindikiza kwenye nyavu.
Bado HFC walikuwa na njaa ya magoli wakifanya mashambulizi ya kila dakika, ndipo kiungo mkabaji Amani alipompatia McDennis pasi aka assist nzuri naye akiwa katima wing ya kulia alisogea kidogo na kuachia shuti kali sana lililomfanga kipa asijue la kufanya wala asione mpira umepita wapi na akashangaa tu umekwama nyavuni.
Alikuwa ni Amani tena aliyepiga assist kwa Mola Jumanne aliyeupokea mpira na kuchomoka mithili ya #TheFlash na kumchungulia kipa amekaaje na akaukwamisha mpira nyavuni.
SupeeLoaf wakarudi tena katika mashambulizi huku mabeki wa HFC wakiwa wamejisahau, alikuwa ni Hamisi tena akipiga shuti la karibu na kumuweza tena kipa namba mbili wa HFC Vincent Andrea aka kaka aka Mratibu.
Man of the match akiwa ni Amani baada ya kutoa Assist 2 katika mchezo huo na kuumiliki vizuri mchezo katika eneo la katikati.
Kipa Vincent Andrea alionesha uwezo mkubwa huku akiokka magoli matatu ya wazi.
Mchezo ulikuwa mzuri sana na hadi FT: HFC 4, SUPERLOAF FC 2.
Comments
Post a Comment