HFC vs SLFC KESHO 10:00 JIONI GENERAL TIRE ARUSHA
HFC vs SLFC KESHO 10:00 JIONI GENERAL TIRE ARUSHA
kwa mara nyingine tena wakazi wa jiji la Arusha na Viunga vyake ama mitaa yake kesho watapata kushuhudia burudani muruuuua ya kabumbu pale miamba wawili na wapinzani wakubwa HFC na SUPER LOAF FC aka SLFC watakapokutana uso kwa uso kuvaana kisoka.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kuvutia hasa ikizingatiwa kuwa timu hizi mbili zikutanapo basi nyasi huumia.
HFC ikiwategemea wachezaji wake mahiri kama Michael aka Scmeichel, John Bayo aka mzee Jomo aka wafula aka Nginja nginja, Vincent Andrea aka kaka aka mratibu, Mrundi, Amani, Elikana aka Modric aka Mezut Ozil aka baba Ali, Adam aka Papaa aka kocha mchezaji, Adam aka Davie the Midfielder, McDennis, Peter aka baba Sydney aka mzee mwenzangu aka Ramos, Mola Jumanne aka mzee wa vichwa, Gerald Gunza aka Mo Salah, #AbelRKay aka #YuleYule aka #TheFlash na wengineo wengi wanatarajiwa kutandaza soka safi na kuhakikisha heshima inabakia nyumbani kwa kugawa kichapo kikali aka dhahama aka gharika.
Wote mnakaribishwa kushuhudia soka safi kwenye viwanja vya General Tire Njiro Arusha.
Comments
Post a Comment