FT: HFC 2-1 QUARTERS FC
FT: HIGHRIDGE FC 2-1 QUARTERS FC
QFC wakawa wa kwanza kuliona lango na kwa kuandika bao lao kunako dk ya 17 kipindi cha kwanza, goli lililodumu kipindi chote cha kwanza.
HFC wakarudi wakiwa wamejipanga sawa sawa na kufanikiwa kusawazisha bao kunako dk ya 9 kipindi cha pili kwa shuti la juu la mbali lililopigwa na Anthony Makunenge na kufanya kuwa 1-1.
HFC wakarudi tena kambani wakiwa na nia moja tu, kukata mzizi wa fitina, kukatokea gongeana moja maridadi na pasi ya mwisho kumkita Molla bin Jumanne aliyemchungulia kipa akiwa amezubaa na kuusukumiza mpira nyavuni na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Kama nilivokuahidi kukuletea matukio mengine
Kukatokea vurugu, #Anderson wa QFC akimrukia kichwa #SHABAN wa HFC na kumtoa damu bila sababu yoyote ile kupewa kadi ya pili ya njano ambayo ilizaa nyekundu na kutolewa nje ya dimba.
#Davie wa HFC akachezewa rafu mbaya na FFU akageuka na kumkunja, wote wawili wakala kadi za manjano.
Kelele nyingi zilitoka kwa wachezaji wa QFC na kudhihirisha kwamba hawaujui mpira wala sheria zake kwani kila mara refa akipiga kipenga cha kuotea wanagoma na kupiga kelele mbovu mbovu.
Midomo ya wachezaji wengi wa HFC ilijaa matusi mengi na kuufanya mchezo kutokuvutia kabisa.
Comments
Post a Comment