HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG 2. MZIZI WA FITINA HAUJANG'OLEWA
HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG FC 2. MZIZI WA FITNA HAUJANG'OLEWA BADO. Katika mpambano wa soka wa kirafiki uliozikutaisha timu za HFC na SunFlag FC uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Genwral Tire imeshuhudiwa mbabe akikosekana baada ya timu hizo kulazimishana droo ya 2-2. Mchezo ulianza kwa kasi sana huku Sunflag Fc wakianza kulisukuma gozi mithili ya club za Arsenal na Barcelona, wakionana kwa pasi nzuri na zenye uhakika wakati huo HFC wakiwa hawana wasiwasi wowote wakiwasoma na kujaribu kuziba nafasi iki wapinzani wao hao wasiweze kuoata penetration yoyote. Mpira ulichezwa kwa muda mrefu sana hasa maeneo ya katikati huku kila upande ukishindwa kupata nafasi ya kupata goli la kutangulia. Wakiwa wamefanya mashambukizi ya mara kwa mara, Sunflag Fc kwa kupitia mkjuwa wa penati walikosa goli na hali kurudi ile ile yaani 0-0. Lakini HFC wakiwa wamejisahau hasa walinzi wake, Sunflag fc wakarudi tena langoni kwa HFC na kufanya shambulizi kali mithili ya Vietnamese army na kupitia mche...