HFC WAANGUKIA PUA. WAKUBALI KICHAPO CHA 3-2 TOKA KWA QUARTERS FC
Highridge FC waangukia pua. Wakubali kichapo cha 3-2 toka kwa Quarters FC Katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa General Tire jijini Arusha, HFC wamekula kipigo kitakatifu toka kwa mahasimu wao na majirani zao Quarters FC. Walikuwa ni HFC walioanza kuliona lango la wapinzani wao baada ya kuonana vizuri huku wakicheza kandanda nzuri mithili ya EPL, alikuwa ni Ackrim akicheza wing ya kushoto aliyeonekana kuwapa shida kubwa mabeki wa QFC kwa mbio na mchezo wake mzuri akiwazidi akili na maarifa basi aliachia cross ndogo iliyomkuta Abel RKay aka #TheFlash akiwa takribani mita 25 ama 26 mpaka 27 akamchungulia kipa amekaaje na kuachia shuti la juu lililomshinda kipa na mpira kutinga nyavuni. Dakika chache baadae, HFC wakapata kona na Abel RKay akaichonga kona fupi na kumpasia Muksini aliyeachia shuti kali na kumbabatiza beki wa QFC na mpira kutinga nyavuni. Mpira uliendelea kuchezwa huku QFC wakilizakama lango la HFC kwa vipindi na hatimaye wakafanikiwa kupata goli la kwanz...