Posts

FT: HFC 2-1 QUARTERS FC

Image
FT: HIGHRIDGE FC 2-1 QUARTERS FC QFC wakawa wa kwanza kuliona lango na kwa kuandika bao lao kunako dk ya 17 kipindi cha kwanza, goli lililodumu kipindi chote cha kwanza.  HFC wakarudi wakiwa wamejipanga sawa sawa na kufanikiwa kusawazisha bao kunako dk ya 9 kipindi cha pili kwa shuti la juu la mbali lililopigwa na Anthony Makunenge na kufanya kuwa 1-1.  HFC wakarudi tena kambani wakiwa na nia moja tu, kukata mzizi wa fitina, kukatokea gongeana moja maridadi na pasi ya mwisho kumkita Molla bin Jumanne aliyemchungulia kipa akiwa amezubaa na kuusukumiza mpira nyavuni na kufanya matokeo kuwa 2-1.  Kama nilivokuahidi kukuletea matukio mengine Kukatokea vurugu, #Anderson wa QFC akimrukia kichwa #SHABAN wa HFC na kumtoa damu bila sababu yoyote ile kupewa kadi ya pili ya njano ambayo ilizaa nyekundu na kutolewa nje ya dimba.  #Davie wa HFC akachezewa rafu mbaya na FFU akageuka na kumkunja, wote wawili wakala kadi za manjano.  Kelele nyingi zilitoka kwa wachezaji wa QFC ...

SUPER FRIDAY MATCH DAY. HFC vs SOWETO FC. GROUND: GENERAL TIRE, ARUSHA. USIKOSE UHONDO

Image
SUPER FRIDAY MATCH DAY. HFC vs SOWETO FC. GROUND: GENERAL TIRE, ARUSHA. USIKOSE UHONDO Tunapenda kuwaalika wapenzi wa soka kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha kuja kushuhudia mpambano mkali na mtamu wa soka kati ya HFC vs SOWETO FC zote za jijini Arusha.  HFC wamejipanga sawa sawia wakiwa na ari, nguvu na nia ya ushindi kuhakikisha mashabiki hawapotezi muda wao bali kushuhudia burudani muruuuwa ya kabumbu safi. Wakiwa chini ya kocha Papaa aka Fidel Castro na kepteni J. Bayo aka mzee Jomo watahakikisha kuwa wapinzania wao hao wanarudi makwao vichwa chini miguu juu mithili ya jogoo aliyechinjwa kwa ajili ya krismasi.  Kwa upande wa SOWETO FC, sio timu ya kubeza Kwani wanacheza mpira mzuri na wa upinzani ya hali ya juu. Wana nguvu na speed nzuri sana. Hivyo mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu kwa pande sote na ya kukata na shoka.  Karibuni woooote mfurahie burudani babukubwa. #AbelRKay #TheFlash

HIGHRIDGE SCHOOL SPORTS BONANZA. GENERAL TIRE GROUND ARUSHA. TOMORROW JULY 14, 2018 FROM 9 AM

Image
HIGHRIDGE SCHOOL SPORTS BONANZA. GENERAL TIRE GROUND ARUSHA TOMORROW JULY 14, 2018. DON'T YOU DARE MISS IT Who prevails? Will it be the Mighty Elephants again? Being the defending champions this time round, having won a previous 12 out of the 16 High ridge school sports day bonanza so far, is number 13 lucky for the Elephants, this pauses to be the lingering question in the minds of the many sports enthuthiasts at Highridge school and the community at Large. Sir Eric Bayo aka Mzee Jomo is charged with the task of maintaining this almost perfect feat so far.. Rhino House is yet to win this tournament, as it has always placed fourth but this time round its a force to be reckoned, Its Patron Sir Gerald Gunza, has transformed this house with his meticulous attention to detail and strong will,  boasting a second place position for the third year running, Sir Gerald aka Faru John seems to be on the verge doing the unthinkable, as was seen on the rehearsals today, are they fourth time luc...

HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG 2. MZIZI WA FITINA HAUJANG'OLEWA

Image
HAKUNA MBABE. HFC 2 SUNFLAG FC 2. MZIZI WA FITNA HAUJANG'OLEWA BADO. Katika mpambano wa soka wa kirafiki uliozikutaisha timu za HFC na SunFlag FC uliopigwa jioni ya leo kwenye dimba la Genwral Tire imeshuhudiwa mbabe akikosekana baada ya timu hizo kulazimishana droo ya 2-2. Mchezo ulianza kwa kasi sana huku Sunflag Fc wakianza kulisukuma gozi mithili ya club za Arsenal na Barcelona, wakionana kwa pasi nzuri na zenye uhakika wakati huo HFC wakiwa hawana wasiwasi wowote wakiwasoma na kujaribu kuziba nafasi iki wapinzani wao hao wasiweze kuoata penetration yoyote. Mpira ulichezwa kwa muda mrefu sana hasa maeneo ya katikati huku kila upande ukishindwa kupata nafasi ya kupata goli la kutangulia. Wakiwa wamefanya mashambukizi ya mara kwa mara, Sunflag Fc kwa kupitia  mkjuwa wa penati walikosa goli na hali kurudi ile ile yaani 0-0. Lakini HFC wakiwa wamejisahau hasa walinzi wake, Sunflag fc wakarudi tena langoni kwa HFC na kufanya shambulizi kali mithili ya Vietnamese army na kupitia mche...

HFC vs SLFC KESHO 10:00 JIONI GENERAL TIRE ARUSHA

Image
HFC vs SLFC KESHO 10:00 JIONI GENERAL TIRE ARUSHA kwa mara nyingine tena wakazi wa jiji la Arusha na Viunga vyake ama mitaa yake kesho watapata kushuhudia burudani muruuuua ya kabumbu pale miamba wawili na wapinzani wakubwa HFC na SUPER LOAF FC aka SLFC watakapokutana uso kwa uso kuvaana kisoka. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kuvutia hasa ikizingatiwa kuwa timu hizi mbili zikutanapo basi nyasi huumia.  HFC ikiwategemea wachezaji wake mahiri kama Michael aka Scmeichel, John Bayo aka mzee Jomo aka wafula aka Nginja nginja, Vincent Andrea aka kaka aka mratibu, Mrundi, Amani, Elikana aka Modric aka Mezut Ozil aka baba Ali, Adam aka Papaa aka kocha mchezaji, Adam aka Davie the Midfielder, McDennis, Peter aka baba Sydney aka mzee mwenzangu aka Ramos, Mola Jumanne aka mzee wa vichwa, Gerald Gunza aka Mo Salah, #AbelRKay aka #YuleYule aka #TheFlash na wengineo wengi wanatarajiwa kutandaza soka safi na kuhakikisha heshima inabakia nyumbani kwa kugawa kichapo kikali aka dhahama aka gharika....

HFC WAANGUKIA PUA. WAKUBALI KICHAPO CHA 3-2 TOKA KWA QUARTERS FC

Image
Highridge FC waangukia pua. Wakubali kichapo cha 3-2 toka kwa Quarters FC Katika mechi iliyopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa General Tire jijini Arusha, HFC wamekula kipigo kitakatifu toka kwa mahasimu wao na majirani zao Quarters FC. Walikuwa ni HFC walioanza kuliona lango la wapinzani wao baada ya kuonana vizuri huku wakicheza kandanda nzuri mithili ya EPL, alikuwa ni Ackrim akicheza wing ya kushoto aliyeonekana kuwapa shida kubwa mabeki wa QFC kwa mbio na mchezo wake mzuri akiwazidi akili na maarifa basi aliachia cross ndogo iliyomkuta Abel RKay aka #TheFlash akiwa takribani mita 25 ama 26 mpaka 27 akamchungulia kipa amekaaje na kuachia shuti la juu lililomshinda kipa na mpira kutinga nyavuni. Dakika chache baadae, HFC wakapata kona na Abel RKay akaichonga kona fupi na kumpasia Muksini aliyeachia shuti kali na kumbabatiza beki wa QFC na mpira kutinga nyavuni. Mpira uliendelea kuchezwa huku QFC wakilizakama lango la HFC kwa vipindi na hatimaye wakafanikiwa kupata goli la kwanz...

SUPER LOAF FC WAINGIA MITINI. WAKWEPA MVUA YA MAGOLI

Image
SUPER LOAF FC WAINGIA MITINI. WAKWEPA MVUA YA MAGOLI. Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na pafukapo moshi pana moto. Hili wameliona SuperLoaf FC na kwa kufwatilia misemo hiyo wakaamua kutoonekana uwanjani.  Baada ya kula kichapo cha goli 4-2 katika dimba la General tire pale walipowatembelea HFC, SuperLoaf FC walionekana kutoridhika na kipigo hicho na kuomba kurudiana Ijumaa ambayo ingefwatia. HFC hawakuwa na hiana bali kuwakubalia na kusema karibuni tena. Jana HFC walionekana muda wote wa jioni wakifanya mazoezi ya hapa na pale huku kikosi chao kikiwa kimekamilika vilivyo wakiwa wamejipanga kutoa dozi nyingine. Lakini mazoezi hayo yalionekana kutokuwa na mwisho baada ya habari kusambaa kuwa SuperLoaf FC hawaji uwanjani. Na baada ya kuhoji nikapata.habari kuwa kutokuja kwao uwanjani ilikuwa ni kuhofia mvua. Mvua waliyoiogopa sio ambayo ilikuwa ikinyesha jana asubuhi na mchana la hasha bali waliogopa mvua ya magoli kwa kukumbuka kipigo walichokipata ijumaa iliyopita wak...